SOKA-KLABU BINGWA-AFRIKA

Taji la klabu bingwa Afrika: Mechi za mzunguko wa kwanza zapigwa

Klabu ya Gor Mahia ilipata bao la dakika za lala salama, kuishinda Nyasa Big Bullets ya malawi bao 1-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika.

Klabu ya Kenya ya Gor Mahia.
Klabu ya Kenya ya Gor Mahia. Twitter. com/ Gor Mahia
Matangazo ya kibiashara

Bernard Ondiek, aliingia uwanjani, na kuisaidia klabu kupata ushindi huo muhimu, katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Michezo wa Kasarani Jumatano usiku.

Ilikuwa ni mechi ya kwanza na muhimu kwa kaimu koch Zedekiah Otieno ambaye, alimwanzisha mchezaji mpya Erisa Ssekisambua kutoka Uganda, akishirikiana na Jacques Tuyisenge pamoja na Kenneth Muguna.

Mechi ya marudiano, itachezwa baada ya wiki moja jijini Blantyre, wiki ijayo.

Matokeo mengine ya mzunguko wa kwanza:

APR Rwanda) 0-0 Club Africain (Tunisia)

Al Hilal (Sudan) 4-0 JKU (Zanzibar)

Al-Merrikh (Sudan) 2-1 Vipers (Uganda)

Simba (Tanzania) 4-1 Mbabane Swallows (Eswatini)

Le Messager Ngozi (Burundi) 0-1 Ismaily (Misri)

Mshindi katika mechi za mzunguko wa awali, atafuzu katika hatua ya kwnaza. Timu ambazo zinasuburiwa katika hatua ya kwanza ni pamoja na Wydad Casablanca, TP Mazembe, Al Ahly, AS Vita Club.