SOKA-MICHEZO-UEFA

Soka: PSG-Manchester United na Lyon-Barça watarajia kujitupa uwanjani katika Ligi ya Mabingwa

Wachezaji wa Paris Saint-Germain katika mazoezi kabla ya mechi yao Ligi ya Mabingwa dhidi ya Liverpool, Septemba 17, 2018.
Wachezaji wa Paris Saint-Germain katika mazoezi kabla ya mechi yao Ligi ya Mabingwa dhidi ya Liverpool, Septemba 17, 2018. Action Images via Reuters/Jason Cairnduff

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza Manchester United na klabu ya Ufaransa ya PSG watajitupa uwanjani kupimana nguvu katika hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Nao Manchester City watamenyana na Schalke ya Ujerumani. Uamuzi huo umetolewa baada ya droo kufanywa.

Paris Saint Germain (PSG) hawajashindwa msimu huu katika ligi ya nyumbani ambapo wanaongoza wakiwa na alama 44 kutoka mechi 16.

Kwa upande wa Schalke wamo nafasi ya 13 Bundesliga na wameshinda mechi nne pekee kati ya 15.

Schalke walimaliza wa pili Kundi D nyuma ya Porto lakini mbele ya Galatasaray na Lovomotiv Moscow.

Timu nyingine ambao zimepangiwa kucheza ni pamoja na Liverpool kukutana na Bayern Munich, Lyon kuvumbuana na Barcelona, huku Ajax wakizipiga na Real Madrid.