MASUMBWI-FLOYD MAYWEATHER-TENSHIN NASUKAWA

Floyd Mayweather amwangusha Tenshin Nasukawa baada ya sekunde 140

Floyd Mayweather Jr akitabasamu baada ya kumwangusha Tenshin Nasukawa baada ya muda mfupi wa kuanza kwa pambano hilo December 31 2018 jijini Tokyo
Floyd Mayweather Jr akitabasamu baada ya kumwangusha Tenshin Nasukawa baada ya muda mfupi wa kuanza kwa pambano hilo December 31 2018 jijini Tokyo PHOTO | RIZIN FF | AFP

Mwanamasumbwi kutoka Marekani Floyd Mayweather alihitaji tu sekunde 140 kumwangusha Mjapan Tenshin Nasukawa katika onyesho la pambano la raundi tatu, lililoandaliwa jijini Tokyo.

Matangazo ya kibiashara

Mayweather ambaye amesema amestaafu kucheza mchezo huo, alikuwa anatabasamu kipindi chote cha pambano hilo fupi na baadaye ya ushindi dhidi ya mpinzani wake anayefahamika sana kwa mchezo wa Kickboxing, alijishinda Dola Milioni 9.

Makonde ya Maywether, yalimlemea Nasukawa ambaye alionekana akitoa machozi, ikambidi kicha wake kurusha taulo jeupe kama ishara kuwa, amesalimu amri.

Katika mapigano 50 aliyopigana, Mayweather mwenye  umri wa miaka 41, ameshinda yote huku akipata mapigano 27 kupitia Knock Out.

Haijawahi kupoteza pigano hata moja.

Miongoni mwa wanamasumbwi maarufu aliyowahi kupambana nao na kushinda ni pamoja na Manny Pacquiao na Conor McGregor.