Pata taarifa kuu
MICHEZO-2019-SOKA-AFRIKA-DUNIA

Matukio makubwa viwanjani mwaka 2019

Uwanja wa Kimataifa wa Al-Wakrah utakaoandaa kombe la dunia mwaka 2022
Uwanja wa Kimataifa wa Al-Wakrah utakaoandaa kombe la dunia mwaka 2022 Reuters
Ujumbe kutoka: Victor Melkizedeck Abuso
2 Dakika

Mwaka 2019, utakuwa na matukio mbalimbali ya kimichezo barani Afrika na kwingineko duniani.

Matangazo ya kibiashara

Kombe la mataifa bingwa barani Afrika:

Fainali ya michuano ya mchezo wa soka kuwania taji la AFCON 2019, itafanyika kati ya tarehe 15 mwezi Juni hadi 13 mwezi Julai.

Mwenyeji anatarajiw akufahamika mapema mwezi Januari.

Kwa mara ya kwanza, mataifa 24 yatashiriki katika fainali hii.

Madagascar na Mauritania zimefuzu kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano haya baada ya kufanya vema katika michuano ya kufuzu mwaka 2018.

Eneo la Afrika Mashariki itawakilishwa na Uganda na Kenya.

Kombe la Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 20:

Makala ya 15, kuwania ubingwa soka kwa vijana wasiozidi miaka 20 barani Afrika, itachezwa kati ya tarehe mbili na 17 mwezi Februari nchini Niger.

Mataifa maneno yanayotarajiwa kushiriki ni pamoja na wenyeji Nigeria, Burkina Faso, Burundi, Ghana, Mali, Nigeria, Senegal na Afrika Kusini.

Kundi A, lina Niger, Afrika Kusini, Nigeria na Ubelgiji, kundi la B lina Senegal, Mali, Burkina Faso, Mali, Senegal na Ghana.

Kombe la Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 17:

Tanzania itakuwa mwenyeji wa fainali ya soka kwa vijana wasozidi miaka 17.

Michuano hiyo, itachezwa jijini Dar es salaam kati ya tarehe 14 hadi 28 mwezi Aprili.

Mataifa manane yatakayoshiriki katika michuano hiyo ni pamoja na wenyeji Tanzania, Morocco, Senegal, Guinea, Nigeria, Cameroon, Uganda inayoshiriki kwa mara ya kwanza na Angola.

Kundi A, linajumuisha Tanzania, Nigeria, Angola na Uganda.

Kundi B, Guinea, Cameroon, Morocco na Senegal.

Kombe la dunia, soka la ufukweni :

Fainali ya 10, ya michuano hii itachezwa nchini Paraquay, kule Amerika Kusini.

Mataifa 16 yatashiriki, wakiwemo wawakilishi wa bara la Afrika Nigeria na Senegal.

Kombe la dunia, mchezo wa raga:

Nchi ya Japan, itakuwa mwenyeji wa fainali ya kombe la dunia katika mchezo wa raga mwezi Septemba.

Mataifa 20 yatawania taji hilo. Afrika itawakilishwa na Afrika Kusini na Namibia.

Mwaka 2015, fainali hii ilifanyika nchini Uingereza na mabingwa watetezi ni New Zealand.

Riadha

Mwaka 2019, utatawaliwa na mashindano kadhaa ya mchezo wa riadha.

Jiji la Aarhus nchini Denmark, itakuwa mwenyeji wa mashindanio ya dunia ya nyika, tarehe 30 mwezi Machi.

Yatakuwa ni mashindano ya 43.

Maelfu ya wanariadha watashiriki katika mbio za Kilomita 10, nane na sita.

Mwisho wa mwezi Septemba hadi mwanzoni mwa mwezi Oktoba, jiji la Doha nchini Qatar litakuwa mwenyeji wa mashindano ya ridha ya dunia.

Mashindano hayo yalifanyika katika uwanja wa Kimataifa wa Khalifa.

Mwaka 2017, mashindano haya yalifanyika jijini London nchini Uingereza.

Kriketi:

Kombe la dunia katika mchezo wa Cricket, litafanyika kati ya mwezi Mei hadi Julai 14 nchini Uingereza na Wales.

Mataifa 10 yatashiriki, huku mechi 48 zikichezwa.

Wawakilishi wa bara Afrika ni Afrika Kusini.

Mabingwa watetezi ni Australia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.