DRC-SOKA

Robert Kidiaba achaguliwa kuwa mbunge DRC

Robert Muteba Kidiaba, kipa wa zamani wa TP Mazembe tangu mwaka 2002.
Robert Muteba Kidiaba, kipa wa zamani wa TP Mazembe tangu mwaka 2002. AFP PHOTO/JUNIOR D.KANNAH

Kipa wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya DRC na klabu ya TP Mazembe Robert Kidiaba, amechaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la mkoa wa Katanga.

Matangazo ya kibiashara

Kidiaba ambaye siku zake alipata umaarufu mkubwa kwa kucheza kwa makalio na kuwafurahisha mashabiki, sasa anakuwa mwanasiasa.

Wakati akicheza soka, Kidiaba mwenye umri wa miaka 42, aliichea timu ya taifa mara 61, tangu mwaka 2002 hadi 2015 lakini pia amekuwa katika klabu ya TP Mazembe, ambako hadi kuchaguliwa kwake katika bunge la nchi yake amekuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo.

Alianza kuonesha dalili za kuwa mwanasiasa mwaka 2015, baada ya kustaafu kucheza soka.