MANCHESTER CITY-WOLVES-SOKA

City washindwa kufikia ndoto yao licha ya kuwaburuza Wolves 3-0

Roger Guedes (kushoto) na Gabriel Jesus, aliyeifungia klabu yake mabao mawili dhidi ya Wolves
Roger Guedes (kushoto) na Gabriel Jesus, aliyeifungia klabu yake mabao mawili dhidi ya Wolves REUTERS/Paulo Whitaker

Manchester City wamepunguza uongozi wa Wolves kwa kuwafunga mabao 3-0, lakini ushindi wa City haukutegemewa na wengi. Wengi walitegemea kuwa Wolves wangeshinda katika mechi hiyo. 

Matangazo ya kibiashara

Gabriel Jesus aliifungia City mabao mawili. Alifunga bao lake la kwanza katika dakika ya 10 ya mchezo.

Katika dakika ya 19 Wolves walipata pigo kubwa baada ya mchezaji wake Willy Boly kufukuzwa uwanjani kwa kuonyeshwa kandi nyekundu kwa kumchezea visivyo Bernardo Silva.

Jesus alianza ufungaji wa mabao dakika ya 10 pale Leroy Sane alipoifikia pasi kutoka kwa Aymeric Laporte na akamwandalia Mbrazil huyo mpira safi na kumuwezesha kufunga.

Bao la pili la City lilifungwa na Jesus katika dakika ya 39 kupitia mkwaju wa penalti baada ya Ryan Bennett kumfanyia madhambi Raheem Sterling katika eneo la hatari.

Katika dakika ya 78 Conor Coady alijifunga na kukamilisha ushindi wa City wa mabao 3-0 dhidi ya Wolves.

Hata hivyo City walikuwa bado wanatafuta magoli zaidi, lakini walimaliza mechi wakiwa bado wanatafuta bao moja kutimiza mabao 100 katika mashindano yote msimu huu.

Wengi wanasema City wamepoteza fursa ya kufikia rekodi walioweka wenyewe msimu wa 2013-14 kwa kuwa klabu ya kwanza kabisa kufikia mabao hayo enzi ya Ligi ya Premia kwa kasi zaidi.