AFCON-CAF-SOKA

Mkusanyiko wa mchezo wa soka barani Afrika

Klabu ya Al Ahly ya Misri ikijiandaa kucheza na Simba FC ya Tanzania
Klabu ya Al Ahly ya Misri ikijiandaa kucheza na Simba FC ya Tanzania CAF Online

Michuano ya hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika, zinanchezwa jioni hii katika viwanja mbalimbali barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Lobi Stars vs Wydad Casablanca -Kundi A

Platinum vs Horoya -Kundi B

TP Mazembe vs Club Africain -Kundi C

Vita Club vs Saoura -Kundi D

Orlando Pirates vs ES Tunis -Kundi B

Al Ahly vs Simba -Kundi D

Siku ya Ijumaa, Mamelodi Sundpwns ya Afrika Kusini, iliendelea kupata ushindi katika mechi muhimu ya kundi A, baada ya kuifunga ASEC Mimosas ya Ivory Coast mabaio 3-1, mjini Pretoria.

Kwa matokeo hayo, mabingwa hao wa mwaka 2016 wanaongoza kundi hili kwa alama sita.

Kundi, C zimesaliana klabu tatu tu, CS Constantine, Club Africain na TP Mazembe baada ya Ismaily ya Misri kufungiwa na Shirikisho la soka barani Afrika, kwasababu ya mashabiki wake kuleta fujo katika mechi ya kwanza dhidi ya Club Africain mwezi uliopita, mjini Ismailia.

Fujo zilianza baada ya Club Africain kuwa kifua mble mabao 2-1.

Taji la Shirikisho:

Klabu ya Horoya ya Guinea
Klabu ya Horoya ya Guinea www.cafonline.com

Michuano ya hatua ya makundi, kuwania taji la Shirikisho barani Afrika itaanza kuchezwa siku ya Jumapili katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

Klabu 16 zimegawanya katika makundi manne, kutafuta taji hili ambalo linashikiliwa na Raja Casablanca ya Morocco.

Kundi A, Hassania Agadir, RS Berkane, Raja Casablanca zote za Morocco na AS Otoho ya Congo Brazaville

Kundi B, Etoile du Sahel, CS Sfaxine kutoka Tunisia, Unugu Rangers ya Nigeria na Salitas ya Burkina Faso.

Kundi C, ZESCO United ya Zambia, Al-Hilal ya Sudan, Asante Kotoko ya Ghana na Nkana ya Zambia.

Kundi D, Gor Mahia ya Kenya, NA Hussein Dey ya Algeria, Petro de Luanda ya Angola na Zamalek ya Misri.

Ratiba ya Jumapili, Februari 3 2019:

Gor Mahia vs Zamalek

ZESCO United vs Nkana

Al Hilal vs Asante Kotoko

Etoile du Sahel vs CS Sfaxien

Enugu vs Salitas

Na Hussein Dey vs Petro de Luanda

Michuano ya vijana wasiozidi miaka 20:

Timu ya taifa vijana wa Niger chini ya miaka 20
Timu ya taifa vijana wa Niger chini ya miaka 20 www.cafonline.com

Makala ya 15 ya michuano ya soka kuwania taji la Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 20, inaanza kuchezwa leo nchini Niger.

Mataifa manane yanayoshiriki ni pamoja na wenyeji Niger, ambao wamepangwa katika kundi la A , na Afrika Kusini, Nigeria na Burundi.

Kundi B, kuna Senegal, Mali, Burkina Faso na Ghana.

Mechi ya ufunguzi ni kati ya wenyeji Niger na Afrika Kusini kuanzia saa Kumi na Mbili na nusu saa za Afrika Mashariki, huku mechi ya pili ikiwa ni kati ya Nigeria na Burundi, saa tatu na nusu usiku.

Mechi hizi zinachezwa katika miji miwili, jiji kuu la Niamey na mji wa Maradi.

Timu nne bora, zitakazofika katika hatua ya nusu fainali, zitalikawakilisha bara la Afrika katika michuano ya kombe la dunia mwaka mwezi Mei nchini Poland.

Vijana wa Burundi, wanawakilisha eneo la Afrika Mashariki na Kati, hii ikiwa ni mara ya pili, baada ya kufanya hivyo mwaka 1995 na kumaliza katika nafasi ya pili.

Wenyeji Niger, wanashiriki kwa mara ya kwanza huku Mali, Ghana na Nigeria zikiwa zimeshiriki zaidi ya mara 10.

Mabingwa watetezi Zambia, hawakufuzu katika michuano hii.