UFARANSA-ARGENTINA-SOKA-AJALI

Ndege iliyombeba Emiliano Sala yapatikana

Picha ya mchezaji wa Argentina Emiliano Sala, alifariki baada ya ndege yake kuanguka baharini tarehe 21 Januari 2019.
Picha ya mchezaji wa Argentina Emiliano Sala, alifariki baada ya ndege yake kuanguka baharini tarehe 21 Januari 2019. REUTERS/Stephane Mahe

Ndege iliyotoweka kwenye anga ya Manche Januari 21, 2019, ambayo ilikuwa ikimsafirisha mchezaji wa Argentina Emiliano Sala pamoja na rubani wake, imepatikana, Shirika la Uingereza linaloendesha uchunguzi wa ajali za ndege (AAIB) limeliambia shirika la Habari la AFP.

Matangazo ya kibiashara

Karibu wiki mbili baada ya kutoweka, ndege iliyomsafirisha mchezaji wa soka Emiliano Sala ambayo ilikuwa ikitokea Ufaransa kuelekea Wales imepatikana, kwenye bahari ya Manche. "Ninaweza kuthibitisha kuwa ndege imepatikana," msemaji wa shirika la Uingereza linaloendesha uchunguzi wa ajali za ndege (AAIB) ameliambia shirika la Habari la AFP.

Hata hivyo, shirika hili halijabainisha eneo na wakati ndege hiyo ilipatikana.

Uchunguzi mpya ulioendeshwa na kampuni ya Blue Water Recoveries (BWR) umewezesha mabaki ya ndege hiyo " kupatikana mapema Jumapili asubuhi," amesema mkuu wa BWR David Mearns.