KENYA-SOKA

AFC Leopards yampata kocha mpya

AFC Leopards imepata kocha mpya Andre Casa Mbungo, raia wa Rwanda. Andre anachukuwa nafasi ya Marko Vasiljevic.
AFC Leopards imepata kocha mpya Andre Casa Mbungo, raia wa Rwanda. Andre anachukuwa nafasi ya Marko Vasiljevic. AFC Leopards SC/twitter.com

Uongozi wa klabu ya AFC Leopards nchini Kenya, umemteua Andre Casa Mbungo raia wa Rwanda kuwa kocha wake mpya, baada ya kujiuzulu kwa Mserbia Marko Vasilejevic kwa sababu ya matokeo mabaya.

Matangazo ya kibiashara

Cassa Mbungo mwenye umri wa miaka 51, ametia saini mkataba wa mwaka mmoja na nusu, kuisaidia klabu hiyo ambayo inashikilia nafasi ya 15 kati ya 18 kufanya vema katika ligi kuu ya soka nchini humo.

Kocha huyo anakuwa mkufunzi wa 26 wa mabingwa hao wa zamani wa soka nchini humo tangu mwaka 2009, na anakuwa kocha wa sita tangu mwaka uliopita.

Kibarua chake cha kwanza kitakuwa siku ya Jumatano, wakati AFC Leopards itakapochuana na Mount Kenya United.