UHISPANIA-MOURINHO-SOKA-HAKI

Jose Mourinho aponea kufungwa jela kwa makosa ya ukwepaji kodi

Jose Mourinho, kocha wa zamani wa Manchester United.
Jose Mourinho, kocha wa zamani wa Manchester United. REUTERS/Pedro Nunes

Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho ameponea kufungwa jela kwa makosa ya ukwepaji kodi nchini Uhispania lakini atalipa faini.

Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Ureno, alipatikana na kosa hilo wakati alipokuwa kocha wa Real Madrid kati ya mwaka 2011 hadi 2012.

Viongozi wa mashataka wameamua kuwa badala ya kumfunga jela, atalipa faini ya karibu Euro Milioni mbili.

Mourihno amepata adhabu hiyo baada ya kushindwa kodi ya Euro Milioni 1.6 mwaka 2011 na nyingine Euro milioni 1.7 mwaka 2012.