Pata taarifa kuu
SOKA-MICHEZO-UEFA

Borussia Dortmund kumenyana na Tottenham Hotspurs

Borussia Dortmund inahitaji kupata ushindi wa angalau mabao 4-0 kwa bila ili kufika katika hatua ya robo fainali.
Borussia Dortmund inahitaji kupata ushindi wa angalau mabao 4-0 kwa bila ili kufika katika hatua ya robo fainali. REUTERS/Ralph Orlowski
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Mechi za mzunguko wa pili, hatua ya 16 kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya, maarufu UEFA zinachezwa leo Jumanne usiku. Timu nne zitajitupa uwanjani.

Matangazo ya kibiashara

Borussia Dortmund ya Ujerumani, itakuwa na kibarua dhidi ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza.

Mechi ya mzunguko wa kwanza, wawakilishi hao wa Ujerumani, walifungwa mabao 3-0 ugenini na hivyo inahitaji kupata ushindi wa angalau mabao 4-0 kwa bila ili kufika katika hatua ya robo fainali.

Real Madrid ya Uhispania nayo itakuwa nyumbani katika uwanja wake wa Bernabeu kucheza na Ajax ya Uholanzi, kutafuta ushindi muhimu wa kusonga mbele. Katika mechi ya kwanza, Real Madrid walipata ushindi wa mabao 2-1.

Klabu hii inakwenda katika mechi hii baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita, kufungwa na watani wao wa jadi Barcelona 1-0 katika mechi ya ligi kuu nchini humo.

Mechi hizi zitachezwa kuanzia saa tano usiku, saa za Afrika Mashariki (sawa na na saa nne usiku saa za Afrika ya Kati).

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.