SOKA-REAL MADRID-ZIDANE-MICHEZO

Soka: Zinedine Zidane arejea tena kuinoa Real Madrid

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa, Zinédine Zidane, Juni 2017.
Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa, Zinédine Zidane, Juni 2017. Reuters / Eddie Keogh Livepic/File Photo

Zinedine Zidane ameteuliwa kwa mara nyingine kuwa kocha wa Real Madrid hadi mwaka 2022. Zidane anajivunia rekodi yake ya kutwaa mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa akiwa na Real Madrid.

Matangazo ya kibiashara

Zidane anarejea wakati klabu hii inakabiliwa na malumbano ya ndani.

Hivi karibuni Real Madrid iliondolewa katika michuano ya Kombe la Ulaya (Ligi ya Mabingwa) na klabu ya Ajax Amsterdam.

Zinedine Zidane aliichezea Real Madrid kati ya mwaka 2001 na 2006 na baadae akaiongoza klabu hiyo kuanzia mwaka 2016 hadi 2018.

Nahodha huyo wa zamani wa Ufaransa anarejea Real Madrid kujaza nafasi ya Santiago Solari aliyeshindwa kupata mafanikio tangu alipotwaa mikoba.

Zidane aliondoka Real Madrid majira ya Kiangazi baada ya kutofautiana na Perez kuhusu mpango wa kuwekeza msimu huu.