KENYA-CAF-SOKA

Gor Mahia yafuzu katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Shirikisho barani Afrika

Klabu ya Kenya ya Gor Mahia.
Klabu ya Kenya ya Gor Mahia. Gor Mahia/Twitter. com

Klabu ya soka ya Gor Mahia nchini Kenya imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Petro Atletico ya Angola katika uwanja wa nyumbani wa Kasarani.

Matangazo ya kibiashara

Gor Mahia, ikiwa na wachezaji tisa uwanjani baada ya wenzao wawili kupewa kadi nyekundu pamoja na kocha wao Hassan Oktay , klabu hiyo ilifanikiwa kufuuzu katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Shirikisho barani Afrika, baada ya kuifunga Petro Atletico ya Angola bao 1-0 katika mechi ya mwisho hatua ya makundi.

Bao hilo la ushindi, lilitiwa kimyani na mshambuliaji Jacques Tuyisenge kupitia mkwaju wa penalti katika dakika ya 58 ya mchuano huo uliochezwa katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi.

Gor Mahia sasa inaugana na Nkana ya Zambia, Etole du Sahel, CS Sfaxien zote kutoka Tunisia, RS Berkane, Hassania Agadir kutoka Morocco, Zamalek ya Misri na Al-Hilal ya Sudan.