Gor Mahia kuwakosa wachezaji wake wanne
Imechapishwa:
Klabu ya Gor Mahia nchini Kenya, itawakosa wachezaji wanne katika mechi ya robo fainali kuwania taji la Shirikisho barani Afrika, baada ya kuiadhibu Petro Atletico ya Angola katika uwanja wa nyumbani wa Kasarani.
Miongoni mwa wachezjai hao ni pamoja na kiungo wa kati Ernest Wendo na Beki Shafik Batambuze walioneshwa kadi nyekundu wakati walicheza na Petro Atletico ya Angola Jumapili iliyopita, mechi ambayo Gor Mahia ilishinda kwa bao 1-0.
Haroun Shakava na naibu Nahodha Jacques Tuyisenge nao watakosa mechi hiyo, kwa sababu wana kadi nyingi za njano.
Gor Mahia inaratajiwa kucheza na RS Berkane, ya Morocco, CS Sfaxien ya Tunisia au Hilal ya Sudan.