Pata taarifa kuu
KENYA-UGANDA-BURUNDI-TANZANIA-AFCON 2019

Mataifa manne ya Afrika Mashariki yafuzu AFCON 2019

Uganda na Tanzania zikimenyana katika mechi muhimu ya kufuzu AFCON 2019 Machi 24 2019
Uganda na Tanzania zikimenyana katika mechi muhimu ya kufuzu AFCON 2019 Machi 24 2019 www.fufa.co.ug
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Kenya, Uganda, Tanzania na Burundi ni mataifa ya Afrika Mashariki na  kutoka ukanda wa CECAFA, yaliyofuzu kucheza fainali ya AFCON mwaka 2019 nchini Misri. 

Matangazo ya kibiashara

Hii haijawahi kutokea katika historia ya mashindano haya makubwa barani Afrika.

Burundi imefuzu kwa mara ya kwanza, baada ya kumaliza katika nafasi ya pili katika kundi C kwa alama 10 nyuma ya Mali.

Uganda nayo ilifuzu mechi moja kabla ya kumalizika kwa mechi za makundi.

Licha ya kuongoza kundi la L kwa alama 13, Tanzania iliifunga mabao 3-0 katika mechi ya mwisho na kufuzu pia kwa kumaliza nafasi ya pili kwa alama nane.

Kenya nayo ilifuzu mechi moja kabla ya kumalizika kwa michuano ya kufuzu kutoka kundi F lililokuwa na timu tatu, baada ya Sierra Leone kufungiwa na FIFA.

Harambee Stars ilifungwa na Ghana bao 1-0 katika mechi ya mwisho jijini  Accra na kufuzu baada ya kumaliza katika nafasi ya pili katika kundi lao kwa alama saba.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.