Pata taarifa kuu
TANZANIA-NIGERIA-SOKA

Tanzania wazamishwa na Nigeria kwa 5-4

Timu ya taifa ya vijana wasiozidi miaka 17 kutoka Tanzania, Serengeti Boys.
Timu ya taifa ya vijana wasiozidi miaka 17 kutoka Tanzania, Serengeti Boys. Getty images
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Wenyeji Tanzania, wameanza vibaya fainali ya kuwania taji la vijana wasiozidi miaka 17 baada ya kufungwa na Nigeria mabao 5-4 katika mechi muhimu ya ufunguzi wa kundi A.

Matangazo ya kibiashara

Mechi ya ufunguzi ilichezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, Nigeria ndio walionza kupata kabla ya Tanzania kusawazisha na hata kuwa mbele lakini hadi kipenga cha mwisho, Nigeria waliibuka washindi,

Mechi nyingine iliyochezwa Jumapili Aprli 14 katika kundi hilo, Angola waliishinda Uganda bao 1-0.

Kwa namna matokeo hayo yalivyo, NIgeria wanaongoza kundi hili kwa alama tatu, wakifuatwa na Angola ambao pia wana alama tatu.

Leo Jumatatu, itakuwa ni zamu ya kundi B, Guinea watacheza na Cameroon kuanzia saa 10 jioni katika uwanja wa Chamazi, lakini baadae Morocco watakabiliana na Senegal.

Mashabiki wamehimizwa kuhudhuria michuano hii kwa wingi kwa sababu hakuna kiingilio.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.