UFARANSA-FFF-SOKA

Mwamuzi mwanamke kuchezesha mechi ya ligi kuu Ufaransa

Mwamuzi wa kwanza mwanamke, Stephanie Frappart, atachezesha mechi ya ligi kuu ya soka nchini Ufaransa, mwishoni mwa wiki hii, na anatarajia kuchezesha mechi nyingine za kimataifa katika miezi miwili au mitatu ijayo.

Stephanie Frappart (katikati) aliteuliwa na Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, kuchezesha mechi ya fainali ya Kombe la Dunia kwa upande wa wanawake wa wasiozidi miaka 20 (U20), nchini Ufaransa mnamo mwaka 2018.
Stephanie Frappart (katikati) aliteuliwa na Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, kuchezesha mechi ya fainali ya Kombe la Dunia kwa upande wa wanawake wa wasiozidi miaka 20 (U20), nchini Ufaransa mnamo mwaka 2018. FFF/Twitter.com
Matangazo ya kibiashara

Stephanie Frappart atachezesha mechi muhimu kati ya Amiens na Strasbourg, kwa mujibu wa Shirikisho la soka nchini humo FFF.

Frappart ana umri wa miaka 35, ana ataweka historia hiyo baada ya kuchezesha mechi za ligue 2 tangu mwaka 2014.

Atachezesha pia michuano ya kombe la dunia itakayofanyika jijini Paris kati ya mwezi Juni na Julai.

Stephanie Frappart aliteuliwa na Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, kuchezesha mechi ya fainali ya Kombe la Dunia kwa upande wa wanawake wa wasiozidi miaka 20 (U20), nchini Ufaransa mnamo mwaka 2018.