CAF yatoa fedha kwa mataifa 24 yaliyofuzu fainali ya AFCON
Imechapishwa:
Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limetoa Dola 260,000 kwa mataifa yote 24 yaliyofuzu kucheza fainali ya Afrika nchini Misri mwezi Juni.
CAF inasema, fedha hizo zinalenga kuyasaidia mataifa hayo kuanza maandalizi ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
Mbali na fedha hizo, CAF imetenga Dola 475,000 kwa timu zitakazoondolewa katika hatua ya makundi lakini huku bingwa akitarajiwa kupata Dola Milioni 4.5.
Mataifa yaliyofuzu katika michuano hiyo ni pamoja na:-
Kundi A, Misri, DRC, Uganda na Zimbabwe.
Kundi B, Nigeria, Guinea, Madagascar na Burundi.
Kundi C, Senegal, Algeria, Kenya na Tanzania.
Kundi D, Morocco, Ivory Coast, Afrika Kusini na Namibia
Kundi E, Tunisia, Mali, Mauritania na Angola.
Kundi F, Cameroon, Ghana, Benin na Guinea-Bissau.