RIADHA-LONDON-KENYA

Eliud Kipchoge aandikisha rekodi mpya mbio za London Marathon

Mwanariadha kutoka nchini Kenya Eliud Kipchoge akishangilia baada ya kumaliza wa kwanza katika mbio za London Marathon zilizofanyika leo nchini Uingereza
Mwanariadha kutoka nchini Kenya Eliud Kipchoge akishangilia baada ya kumaliza wa kwanza katika mbio za London Marathon zilizofanyika leo nchini Uingereza AFP

Mwanariadha wa Kenya, Eliud Kipchoge ameweka rekodi mpya ya kushinda mbio za London Marathon mara nne mtawalia.  

Matangazo ya kibiashara

Kipchogfe ametetea ubingwa wake kwa kuweka rekodi ya aina yake akiwashinda wapinzani wake kwa karibu mwendo wa kilomita tatu.

Kipchoge ametumia saa 2:2:37 na kuvunja rekodi yake aliyoweka mwaka 2016 katika mbio hizo kwa kutumia muda wa saa 2:3:5.

Wanariadha kutoka Ethioipia Mosinet Geremew and Mule Wasihun wameshika nafasi ya pili na ya tatu.

Mwaka wa jana Kipchoge alitajwa kuwa mwanariadha mashuhuri duniani.

Mwanariadha ria wa Uingereza, Mo Farah a,mbaye hivi karibuni ameingia kwenye mzozo na mwanariadha Haile Gebrselassie alimaliza katika nafasi ya tano