LA LIGA

Polisi nchini Hispania inawashikilia watu kadhaa kwa tuhuma za upangaji matokeo

Mshambuliaji wa FC Barcelona, Lionel Messi akishangilia moja ya magoli aliyofunga katika moja ya mechi za ligi kuu ya Uhispania.
Mshambuliaji wa FC Barcelona, Lionel Messi akishangilia moja ya magoli aliyofunga katika moja ya mechi za ligi kuu ya Uhispania. REUTERS/Sergio Perez

Polisi nchini Hispania imewakamata watu kadhaa kama sehemu ya uchunguzi kuhusu taarifa za upangaji matokeo kwenye mezi za Laliga.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa sasa na wachezaji wa zamani pamoja na wakurugenzi wa vilabu kutoka katika ligi mbili kubwa nchini humo wamekamatwa kwa mahojiano.

"Hatua ya polisi imekuja baada ya uwepo wa malalamiko ya uwezekano wa upangaji matokeo kutoka kwa waendesha ligi kuu hadi kwa mamlaka za nchi hiyo," amesema msemaji wa La Liga.

La Liga pia iliripoti mechi takribani nane ambazo zinao uwezekano kuwa matokeo yake yalipangwa.

"Katika msimu wa 2018/2019 La Liga iliwasilisha malalamiko 8 kwa kamishna wa polisi na mahakama kutokana na vitendo vinavyohusiana na upangaji matokeo katika ligi kuu na ligi zile za chini ambapo wachezaji wa zamani na viongozi wamehusika," imesema taarifa ya La Liga.

La Liga imesema pia imeorodhesha majina ya wachezaji kutoka katika ligi za daraja la chini ili wapewe adhabu kutokana na kubainika kuwa walishiriki kicheza kamari katika baadhi ya mechi.

La Liga kwenye taarifa yake imesema inawashukuru Polisi kwa hatua za haraka walizochukua kujaribu kudhibiti kile ilichosema ni mtandao haramu unaojihusisha na ushawishi wa mechi.