SOKA-CAF-KLABU BINGWA-WYDAD-ESPERANCE

Esperance na Wydad Casablanca kurudia fainai ya klabu bingwa Afrika

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limetangaza kuwa fainali ya mchezo wa soka kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika kati ya Esperance de Tunis ya Tunisia, na Wydad Casablanca ya Morocco, itarudiwa tena.

Esprance de Tunis waliposherehekea taji la klabu binwa Afrika mwaka 2019
Esprance de Tunis waliposherehekea taji la klabu binwa Afrika mwaka 2019 www.cafonline.com
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kikao cha dharura cha Kamati kuu ya CAF kilichofanyika jijini Paris nchini Ufaransa, uongozi wa soka barani Afrika umeamua fainali hiyo itachezwa katika uwanja huru, baada ya kumalizika kwa fainali ya mataifa bingwa barani Afrika itakayomalizika mwezi Julai nchini Misri.

Esperance imeagizwa kurejesha kombe iliyokabidhiwa baada ya fainali tata iliyoshinda bao 1-0 mjini Rades, baada ya sare ya bao 1-1 katika fainali ya kwanza.

Wydad Casablanca ilikataa kuendelea na mchuano huo, baada ya bao la kusawazisha lililofungwa na Walid El Karti katika dakika 59 kukataliwa na mwamuzi wa kati kutoka Gambia, Papa Gassama.

Hali ilikuwa mbaya zaidi, baada ya kubainika kuwa mtambo wa kieletroniki wa kumsaidia refarii kufanya maamuzi VAR,kutoweza kutoa msaada unaohitajika.

Ripoti zinasema kuwa waamuzi na maafisa wa soka wa klabu ya Esperance de Tunis, walifahamu kuwa mtambo wa VAR ulikuwa haufanyi kazi lakini wachezaji wa timu zote mbili hawakuwa na taarifa hizo.

Rais wa CAF Ahmad Ahmad amesema uamuzi huu uliafikiwa kwa pamoja na Kamati Kuu ya Shirikisho hilo.