FIFA-KOMBE LA DUNIA-UFARANSA

Timu za Afrika zaelemewa katika fainali za kombe la dunia za wanawake nchini Ufaransa

Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Ufaransa wakishangilia baada ya kupata ushindi dhidi ya Nigeria 17 Juni 2019
Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Ufaransa wakishangilia baada ya kupata ushindi dhidi ya Nigeria 17 Juni 2019 FIFA

Fainali za Kombe la dunia za wanawake zinazoendelea nchini Ufaransa zimnaelekea kutamatika hatua ya makundi huku mataifa ya Afrika yakishindwa kufua dafu. 

Matangazo ya kibiashara

Afrika Kusini ilinyukwa mabao 4-0 na Ujerumani katika mechi ya mwisho ya kundi B ambalo limeshuhudia Ujerumani, China na Korea Kusini zikifuzu 16 bora.

Nigeria yenye alama tatu katika kundi A inaweza kupata tiketi hiyo na kuungana na Ufaransa na Norway ambazo zimeshakata tiketi ya kucheza hatua hiyo.

Jana Nigeria ilifun gw ana Ufaransa bao 1-0.

Kundi C Italia na brazil zimeshafuzu hatua hiyo kabla ya mechi za mwisho za hatua ya makundi zinachezwa leo kwa Jamaica kuchuana na Australia na Italia kupepetana na Brazil.

Alhamisi mechi za hatua ya makundi zitafikia tamati kwa Marekani kuchuana na Sweden na Cameroon kucheza na Chile.

Zilizofuzu 16 bora

Marekani, Chile, England, Brazil, Italia, China, Australia, Argentina, Sweden, Ujerumani, Australia na wenyeji Ufaransa