Pata taarifa kuu
SENEGAL-AFCON-SADIO MANE

Sadio Mane kukosa mechi dhidi ya Tanzania

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Senegal, Sadio Mane
Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Senegal, Sadio Mane BBC
Dakika 2

Senegal itamkosa mshambuliaji matata, wakati itakapoanza kampeni ya kutafuta ubingwa wa soka barani Afrika siku ya Jumapili dhidi ya Tanzania.

Matangazo ya kibiashara

Mane mwenye umri wa miaka 27, anatumia adhabu ya kutocheza mechi moja katika mashindano haya, baada ya kupata kuoneshwa kadi mbili za njano wakati wa mechi ya mwisho ya kufuzu katika michuano hii.

Kocha wa Senegal Aliou Cisse anasema hana wasiwasi wowote na kutokuwepo kwa Mane, kwa kile anachosema kuwa kikosi chake ni imara.

Wakati wa fainali ya mwaka 2015 nchini Equitorial Guinea, Mane pia alikosa mechi ya kwanza dhidi ya Senehal wka sababu kipindi hicho alikuwa anasumbuliwa na jeraha.

Tanzania ambayo imerejea katika michuano hii mara ya kwanza baada ya miaka 39, inatarajiwa kupambana kupata ushindi muhimu dhidi ya Senegal ambayo inaorodhesa ya 22 duniani dhidi yao ambayo ni ya 131.

Mechi nyingine inayosubiriwa katika kundi hili la C ni kati ya Kenya na Algeria.

Algeria ambao wamekuwa hawafanyi vizuri katika michuano hii, wanajivunia mshambuliaji Baghdad Bounedjah, ambaye ameifungia klabu yake ya Al Sadd nchini Qatar mabao 39 katika mechi 21, alizocheza msimu uliopita.

Kenya nayo imerejea katika michuano hii baada ya miaka 15, na miongoni mwa wachezaji wanaotegemewa ni nahodha Victor Wanyama anayecheza katika klabu ya Tottenham Hotspurs nchini Uingereza.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.