OLIMPIKI-ITALIA-IOC

Italia yashinda uenyeji wa michuano ya olimpiki ya majira ya joto 2026

Rais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki, Thomas Batch akionyesha barua ya kuthibitisha miji ya Milan na Cortina kuandaa michuano ya olimpiki ya majira ya joto 2026
Rais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki, Thomas Batch akionyesha barua ya kuthibitisha miji ya Milan na Cortina kuandaa michuano ya olimpiki ya majira ya joto 2026 EPA

Mji wa Milan na Cortina d'Ampezzo imetangazwa kuwa waandaaji wa michuano ya olimpiki na ile ya walemavu paralimpiki ya majira ya joto mwaka 2026.

Matangazo ya kibiashara

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC imeipatia Italia tenda hiyo baada ya kuipiku Mji wa Stockholm Sweden.

Rais wa OIC Thomas Batch ameipongeza Italia baada ya miji yake kushinda uandaaji wa mashindano hayo.

Miji mingine iliyokuwa ikiwania kuandaa michuano hiyo ni Graz Austria, Calgary Canada, Sion Uswisi na Mji wa Saporo uliopo Japan.