AFCON 2019-BURUNDI-MADAGASCAR

Burundi yakata matumaini ya kuendelea AFCON baada ya kupigwa na Madagascar

Kikosi cha timu ya taifa ya Burundi Intamba mu Rugamba.
Kikosi cha timu ya taifa ya Burundi Intamba mu Rugamba. RFI-KISWAHILI

Timu ya taifa ya Madagascar, “Barea”, iliichapa Burundi 1 – 0. Bao hilo limeiweka timu hiyo katika ukingo wa kufuzu katika hatua ya 16 za mwisho kutoka Kundi B.

Matangazo ya kibiashara

Madagascar inahitaji sare dhidi ya Nigeria ili kuwa na uhakika wa kupenya, au Guinea ikose kuishinda Burundi.

Madagascar inaweza pia kufuzu kama mojawapo ya timu bora za nafasi ya tatu kwenye makundi.

Timu ya Taifa ya Burundi chini ya Kocha Olivier Niyungeko ... Intamba mu Rugamba ipo kundi B pamoja na Madagascar, Guinea, na Nigeria.

Kwa upande mwengine timu ya taifa ya soka ya Kenya imepata ushindi wake wa kwanza, katika michuano ya kuwania taji la bara Afrika inayoendelea nchini Misri, baada ya kufunga majirani zao Tanzania mabao 3-2.

Harambee Stars ilitoka nyuma na kupata ushindi huo muhimu, katika pambano la timu hizo za Afrika Mashariki ambalo lilizua hisia nyingi kuelekea katika mchuano huo.

Michael Olunga alikuwa nyota wa Kenya, baada kuifungia mabao mawili, baada ya Johanna Ommolo kuisawazishia nchi yake bao la pili.

Tanzania walianza vema kwa kupata bao la mapema kupitia Saimon Msuva, huku nahodha Mbwana Samatta akifunga bao la pili kabla ya kipindi cha mapumziko.

Mechi ya mwisho Kenya itacheza na Senegal, kutafuta ushindi au sare ili kufuzu katika hatua ya 16 bora huku Tanzania ambayo imepoteza mechi mbili, ikisalia kumaliza kazi na Algeria.