AFCON 2019: KENYA-TANZANIA

Olunga aweka sehemu nzuri timu yake, Tanzania waangusha kilio

Michael Olunga alikuwa nyota wa Kenya, baada kuifungia timu yake mabao mawili, baada ya Johanna Ommolo kuisawazishia nchi yake bao la pili.
Michael Olunga alikuwa nyota wa Kenya, baada kuifungia timu yake mabao mawili, baada ya Johanna Ommolo kuisawazishia nchi yake bao la pili. Willis Raburu/Twitter.com

Timu ya taifa ya soka ya Kenya imepata ushindi wake wa kwanza, katika michuano ya kuwania taji la bara Afrika inayoendelea nchini Misri, baada ya kufunga majirani zao Tanzania mabao 3-2.

Matangazo ya kibiashara

Harambee Stars ilitoka nyuma na kupata ushindi huo muhimu, katika pambano la timu hizo za Afrika Mashariki ambalo lilizua hisia nyingi kuelekea katika mchuano huo.

Michael Olunga alikuwa nyota wa Kenya, baada kuifungia mabao mawili, baada ya Johanna Ommolo kuisawazishia nchi yake bao la pili.

Tanzania walianza vema kwa kupata bao la mapema kupitia Saimon Msuva, huku nahodha Mbwana Samatta akifunga bao la pili kabla ya kipindi cha mapumziko.

Mechi ya mwisho Kenya itacheza na Senegal, kutafuta ushindi au sare ili kufuzu katika hatua ya 16 bora huku Tanzania ambayo imepoteza mechi mbili, ikisalia kumaliza kazi na Algeria.