AFCON 2019-SENEGALI-KENYA-TANZANIA

Kenya yafungwa na Senegal Tanzania yarejeshwa nyumbani

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars.
Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars. youtube

Timu ya taifa ya Senegal itakutana na Uganda katika mzunguko wa nane wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2019, Julai 5 jijini Cairo. Senegal imeifunga Kenya 3-0 katika kundi C.

Matangazo ya kibiashara

Senegal wametinga hatua ya nane ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 na tayari wanajianda kumenyana na Uganda Julai 5.

Timu ya taifa ya Senegal imetetea nafasi yake katika duru ya pili ya michuano ya AFCON 2019 dhidi ya Kenya na hivyo hivyo kufuzu miongoni mwa timu 16 bora.

Kenya inaweza ikafuzu kama timu ya tatu bora ikitegemea matokeo katika mechi ya mwisho katika kundi E and F.

Katika mechi nyingine Tanzania imefungishwa virago na Algeria.

Na Jamhuri ya Kiemokrasia ya Congo DRC inaweza kufuzu katika kundi A ikiwa na goli moja zaidi, kulingana na matokeo ya Jumatatu.