AFCON-MISRI-SOKA

AFCON 2019: Timu 16 kucheza mzunguko wa nane Misri

Wachezaji wa Madagascar wakionyesha furaha yao baada ya bao lao dhidi ya Burundi katika mzunguko wa kwanza.
Wachezaji wa Madagascar wakionyesha furaha yao baada ya bao lao dhidi ya Burundi katika mzunguko wa kwanza. Suhaib Salem/Reuters

Timu 16 zilizopata tiketi ya kuingia mzunguko wa nane wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 inayoendelea nchini Misri, ambayo inaanza Ijumaa Julai 5 hadi Julai 8, tayari zimepangwa kucheza kwa makundi.

Matangazo ya kibiashara

Algeria, Morocco, Misri, ambao walishinda mechi zao tatu kwa mzunguko wa kwanza, wanasubiriwa kwa hamu na gamu kuona watafanya nini katika mzunguko huo.

Baada ya mechi 36 tangu kuanza kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Misri, tayari timu 16 zilizotinga katika mzunguko wa nane zimepangwa kwa makunndi.

Algeria, ambao wanaendelea kufanya vizuru nchini Misri, watakutana na Guinea, ambayo wamepita kwa bahati nasibu, baada ya kumaliza watatu katika Kundi B.

Nigeria, ambao walimaliza wa pili katika kundi B baada ya kupigwa na Madagascar, watamenyana na Cameroon.

Morocco watapepetana na Benin, ambao walimaliza watatu katika kundi lao. Benin wamepata nafasi hiyo baada ya kutoka sare dhidi ya Cameroon Jumanne (Julai 2) (0-0).

Madagascar, waliowashangaza wengi katika mzunguko wa kwanza, watapepetana dhidi ya DRC. Côte d'Ivoire, mabingwa wa Afrika mwaka 2015 nchini Equatorial Guinea watamenyana dhidi ya Mali.

Misri, wenyeji wa michuano hiyo, watakipiga dhidi ya Afrika Kusini.

Ratiba ya mzunguko wa 16 Kombe la AFCON 2019:

Ijumaa, Julai 5

Morocco - Benin

Uganda - Senegali

Jumamosi, Julai 6

Nigeria - Cameroon

Misri - Afrika Kusini

Jumapili, Julai 7

Madagascar - DRC

Algeria - Guinea

Jumatatu, Julai 8

Mali - Ivory Coast

Ghana - Tunisia