MISRI-AFCON-AFRIKA KUSINI

Wingu zito latanda soka la Misri

Matokeo ya kufurushwa katika hatua ya 16 ya fainali za Afrika zinazoendelea nchini Misri yanaendelea kulitikisa soka la taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.

Mohammed Salah akiwa katika hali ya huzuni baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Afrika Kusini
Mohammed Salah akiwa katika hali ya huzuni baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Afrika Kusini AFP
Matangazo ya kibiashara

Misri ilibandikwa bao 1-0 na Afrika Kusini na kuondolewa katika fainali hizo kubwa za mchezo wa kandanda barani Afrika, bao la dakika ya 85 na mshambuliaji Thembinkosi Lorch.

Rais wa chama cha soka nchini Misri Hani Abou Rabi alimfuta kazi kocha Janvier Aguirre ounde baada ya mchezo huo huku naye akiutangaza kujiuzulu baadaye kidogo.

Ni jambo la nadra sana kutokea kwa uwajibikaji wa namna hii katika kandanda barani Afrika.

Awali, Kocha Aguirre raia wa Mexico alisema anabeba lawama zote kufuatia kipigo ilichopata timu yake ambacho kimewasononesha maelfu ya mashabiki wa soka wa taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.

Lakini je utamaduni huo utaenziwa na mamlaka nyingine za soka katika mataifa ya Afrika, ni suala la kusubiri wakati huu fainali zikiendelea