AFCON 2019-UGANDA-SOKA

Kocha wa timu ya taifa ya Uganda ajiuzulu

Meneja wa timu ya taifa ya Uganda, Cranes, Sébastien Desabre, raia wa Ufaransa, ameamua kujiuzulu kwa ridhaa yake kwenye nafasi hiyo, siku mbili baada ya timu yake kuondolewa katika michuano ya AFCON dhidi ya Senegal.

Timu ya taifa ya Uganda, Cranes, chini yaukofunzi wa Sébastien Desabre, ilishirki michuano ya AFCON 2019 hadi katika mzungko wa 16.
Timu ya taifa ya Uganda, Cranes, chini yaukofunzi wa Sébastien Desabre, ilishirki michuano ya AFCON 2019 hadi katika mzungko wa 16. RFI/ Pierre-René Worms
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imethbitishwa na Shirikisho la Soka nchini la Uganda (Fufa).

Hata hivyo FUFA imekaribisha jitihada za Sébastien Desabre na kutoa mchango wake katika maendeleo ya soka nchini Uganda.

''FUFA inatoa shukrani kwa mchango wa Desabre katika maendeleo ya soka la Uganda na timu ya Uganda Cranes'' shirikisho la Soka nchini Uganda limesem akatika taarifa yake.

Wakati huo huo Fufa imesema itamtangaza kocha mpya 'siku zijazo'baada ya Desabre kuondoka huku akiwa amebakiwa na miezi mitano kumaliza mkataba wake.

Uganda iliaga michuano ya AFCON baada ya kufungwa bao 1-0 na Senegal jijini Cairo siku ya Ijumaa katika mchezo wa hatua ya 16 bora.

Desabre, alisaini mkataba wa miaka miwili kuinoa timu ya taifa ya Uganda, Cranes, mwezi Desemba mwaka 2017.