AFCON 2019-ROBO FAINALI

AFCON 2019:Timu nane zatinga robo fainali

Benin watinga robo fainali, AFCON 2019.
Benin watinga robo fainali, AFCON 2019. Suhaib Salem/Reuters

Mzunguko wa nane wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2019, umemalizika, na sasa mechi nne zinatarajiwa kupigwa katika hatua ya robo fainali Julai 10 na 11.

Matangazo ya kibiashara

Mataifa 24 ndio yalishiriki michuano hiyo tangu kuanza kwa ndinga hiyo Juni 21. Na sasa zimebaki tu timu 8. Mzunguko wa nanae umelilizika Jumatatu Julai 8, kwa ushindi wa Cote d'Ivoire dhidi ya Mali (1-0) na ushindi wa Tunisia dhidi ya Ghana (1-1) baada ya Tunisia kuwa kuingiza mikwaju ya penalti 5 dhidi ya 4 za Ghana.

Timu zitakazocheza katika hatua ya robo fainali tayari zinajulikana. Timu nane ndizo zimetinga katika hatua hiyo ikiwa ni pamoja na Benin, Senegal, Nigeria, Afrika Kusini, Madagascar, Algeria, Cote d'Ivoire na Ghana.

Senegal ambayo iliifunga Uganda 1-0 na itamenyana na Benin ambayo iliikwamisha Morocco baada ya kutoka sare ya 1-1, na kufuatia mikwaju ya penalti ambapo Benin iliingiza mikwaju 4 dhidi ya 1 ya Morocco.

Nigeria iliyowaondoa Cameroon itakutana na Afrika Kusini ambayo iliwakwamisha Misri kwa 1-0.