AFCON-SENEGAL-ALGERIA-SOKA

AFCON 2019: Riyad Mahrez aipatishia ushindi Algeria na kutinga fainali

Wachezaji wa Algeria waonesha furaha yao baada ya ushindi wao dhidi ya Nigeria.
Wachezaji wa Algeria waonesha furaha yao baada ya ushindi wao dhidi ya Nigeria. Amr Abdallah Dalsh/Reuters

Riyad Mahrez ameipatishia timu yake ya Algeria bao la ushindi na kutinga fainali za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, mchuano uliochezwa Jumapili (Julai 14) jijini Cairo, nchini Misri. Algeria imefunga mabao 2-1 dhidi ya Nigeria.

Matangazo ya kibiashara

Bao la ushindi la Algeria limefungwa katika dakika ya 50 kabla ya muda wa ziada wa dakika tano kuingia.

Algeria ndio walianza kuona lango la Nigeria katikakipindi ch kwanza, kabla ya Nigeria kusawazisha katika kipindi cha pili. Nigeria walikuwa na matuamani kwamba watacheza katika kipindi cha lala salama lakini Mahrez amewakata kiu na kujikuta wanazamishwa katika dakika ya 90.

Katika mchezo mwengine Senegal imeifunga Tunisia 1-0.

Goli la kujifunga la Tunisia katika muda wa nyongeza limewavusha Sengal mpaka hatua ya fainali ya kombe la Mataifa ya Africa (AFCON) kwa mwaka 2019.

Ushindi ulipatikana kwa Senegal ndani ya dakika 30 za nyongeza.

Hii ni mara ya pili kwa Senegal kutinga hatua ya fainali. Mara ya kwanza ikiwa 2002 ambapo walipoteza kwa mikwaju ya penati dhidi ya Cameroon.

Mechi ya fainali itachezwa siku ya Ijumaa usiku wiki hii.