Waalgeria waendelea kusherehekea ushindi wao
Imechapishwa:
Maelfu ya mashabiki wa timu ya taifa ya soka ya Algeria wanaendelea kushangilia ushindi wa timu yao dhidi ya Nigeria. Algeria imetinga fainali baada ya kuilaza Nigeria 2-1 katika mchunao wa nusu fainali wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2019) uliochezwa jaan Jumapili Julai 14.
Baada ya miaka 29 timu ya taifa ya soka ya Algeria kutoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, hatimaye imetinga fainali na itacheza na Senegal siku ya Ijumaa usiku wiki hii. Wafuasi wa timu hiyo wameendelea kusherehekea ushindi wao katika miji mbali mbali ya Ufaransa, ikiwa ni pamoja na Paris, Lyon na Marseille.
Matukio mbalimbali yameripotiwa katika miji ya Paris, Lyon na Marseille, baada ya ushindi wa Algeria dhidi ya Nigeria (2-1). Furaha na makabiliano vimeripotiwa, huku watu kadhaa wakikamatwa katika mji wa Marseille, baada ya kukiuka hatua iliyochukuliwa na vikosi vya usalama ya kuingia katika eneo la Vieux-Port.
Mchezaji Riyad Mahrez amejizolea sifa kutoka kwa mashambiki wa timu ya taifa ya soka ya Algeria ndani na nje ya Algeria.
Riyad Mahrez ndiye alifunga bao la ushindi katika dakika ya 90 na kufuta matumaini ya Nigeria.
Ā