AFCON-ALGERIA-SENEGAL-SOKA

AFCON 2019: Mechi ya fainali kuchezwa kati ya Senegal na Algeria

Mpira rasmi wa AFCON 2019, katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa mashindano, Juni 20, 2019, Cairo.
Mpira rasmi wa AFCON 2019, katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa mashindano, Juni 20, 2019, Cairo. MOHAMED EL-SHAHED / AFP

Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 17, hatimaye Senegal imeingia katika hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2019). Mashabiki wa Simba wa Teranga wana hamu ya kuona mechi hiyo ikianza, huku wakiwa na matumaini ya kutwaa kombe leo Ijumaa!

Matangazo ya kibiashara

Pazia la mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Afcon 2019 litafungwa mjini Cairo kwa kuandaliwa fainali ya kukata na shoka. Afrika Magharibi inakutana na Afrika Kaskazini

Katika mchuano wa fainali wa leo Ijumaa, Senegal watamenyana na Algeria.

Hata hivyo Algeria wameapa kuondoka na kombe la michuano hiyo.

Mashabiki wa timu ya taifa ya Soka ya Algeria wamesema wako tayari kuwashinda Senegal kama walivyowashinda Nigeria wiki moja iliyopita.

Algeria ilitinga fainali baada ya Riyad Mahrez kufunga freekick safi sana katika dakika ya tano ya muda wa majeruhi na kupata ushindi wa 2 – 1 dhidi ya Nigeria. Senegal nao walifuzu baada ya ushindi wa 1 – 0 dhidi ya Tunisia katika muda wa ziada baada ya mechi kukamilika bila kufungana katika muda wa ziada.

Algeria wanawinda Kombe la Afrika kwa mara ya pili na lao la kwanza katika karibu miaka 30. Senegal wanawinda taji lao la kwanza la Afrika baada ya miaka 54 ya kujaribu.

Mashabiki wa timu ya taifa ya soka ya Senegal Dakar wakati timu yao ikicheza hatua ya nusu fainali dhidi ya Tunisia Julai 14, 2019.
Mashabiki wa timu ya taifa ya soka ya Senegal Dakar wakati timu yao ikicheza hatua ya nusu fainali dhidi ya Tunisia Julai 14, 2019. REUTERS/Zohra Bensemra