AFRIKA-KIKAPU-KENYA-TUNISIA

Kikapu: Kenya kucheza na Tunisia nusu fainali ya kutafuta ubingwa wa Afrika

Wachezaji wa timu ya taifa ya Kenya, mchezo wa kikapu Julai 25 2019
Wachezaji wa timu ya taifa ya Kenya, mchezo wa kikapu Julai 25 2019 www.fiba.basketball

Timu ya taifa ya mchezo wa kikapu kwa upande wa wanaume, imefuzu katika hatua ya nusu fainali, kuwania taji la bara Afrika katika michuano inayoendelea nchini Mali.

Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha Kenya kinachofahamika kama Morans, ilifika katika hatua hiyo baada ya kuishinda Tunisia kwa vikapu 82-76.

Kenya sasa itamenyana na Morocco katika hatua ya nusu fainali siku ya Alhamisi jijini Bamako.

Wachezaji wa Kenya wakiongozwa na nahodha Griffin Ligare, wameonesha kiwango cha juu  katika mashindano haya makubwa barani Afrika.

Ushindi mwingine muhimu wa Kenya, ulikuwa dhidi ya Ivory Coast kwa vikapu 85-83.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itemenyana na Angola katika mechi nyingine ya nusu fainali siku ya Alhamisi.

Mataifa mengine yanayoshiriki katika michuano hii ni pamoja na Algeria, DRC, Mali, Algeria, Misri, Morocco, Chad, Guinea, Nigeria, Cote d'Ivore na Tunisia.