KENYA-DRC-KIKAPU-AFRIKA

Kenya na DRC kucheza fainali ya kuwania taji mchezo wa kikapu barani Afrika

Wachezaji wa Kenya
Wachezaji wa Kenya www.fiba.basketball

Kenya na DRC zitapambana katika fainali ya mchezo wa kikapu kuwania taji la bara Afrika kwa upande wa wanaume, mchezo utakaochezwa siku ya Jumamosi, jijini Bamako nchini Mali.

Matangazo ya kibiashara

Wachezaji wa Kenya waliandikisha historia katika mashindano hata baada ya kufuzu katika hatua hiyo ya fainali, iliyokuja baada ya kuishinda Morocco kwa vikapu 96 kwa 66 katika mechi ya nusu fainali siku ya Ijumaa.

Fainali ya Jumamosi inatarajiwa kuwa ngumu kwa sababu nch zote mbili zilikutana katika hatau ya makundi lakini DRC ilipata ushindi kwa vikapu 82-65 katika mechi ya kwanza.

Safari ya kuelekea fainali, haikuwa rahisi, Kenya walipata ushindi mwembamba wa vikapu 85-83 dhidi ya Ivory Coast katika hatua ya 16 bora na baadaye ikailemea Tunisia kwa vikapu 82-76 katika hatua ya robo fainali.

DRC haijafungwa katika safari ya kutafuta ubingwa wa taji hili.