BRAZILI-NEYMAR-SOKA

Polisi: Hatuna ushahidi wa kumshtaki Neymar kwa ubakaji

Neymar,mchezaji nyota wa Brazili.
Neymar,mchezaji nyota wa Brazili. REUTERS/Grigory Dukor

Polisi wa Brazili wamebaini baada ya uchunguzi kwamba hakuna ushahidi wa kutosha kumshtaki nyota wa mpira wa miguu Neymar kwa kumbaka msichana mmoja wa Brazili mnamo mwezi Mei jijini Paris, nchini Ufaransa, ofisi ya mwendesha mashtaka ya Sao Paulo imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi wa polisi, awamu ya kwanza ya kesi hiyo, umekwisha na ripoti inatarajiwa kuwasilishwa Jumanne wiki hii kwa mwendesha mashtaka, ambaye atakuwa na siku 15 kuamua ikiwa Neymara atafunguliwa mashitaka au la, msemaji wa Mwendesha Mashtaka wa Sao Paulo ameliambia shirika la Habari la AFP.

Mshambuliaji nyota wa Paris Saint-Germain anatuhumiwa na Najila Trindade Mendes de Sousa, mnenguaji kutoka Brazili, kwa kumbaka mnamo Mei 15 katika hoteli ya jini Paris, nchini Ufaransa. Neymar anadai kuwa hana hatia na anadai kwamba alitembea kimapenzi na mwanamke huyo baada ya kuafikiana.

Polisi wa Sao Paulo, ambapo Najila Trindade aliwasilisha malalamiko yake dhidi ya Neymar wiki mbili baada ya tukio hilo la kubakwa, inabaini kwamba hakuna ushahidi wa kutosha kumshtaki Neymar kwamba alimlazimisha mwanamke huyo kufanya ngono bila ridhaa yake na kumyanyasa kimwili.

Neymar alihojiwa mnamo Juni 13 katika kituo cha polisi cha Sao Paulo. Najila Trindade alisikilizwa mara mbili, pia huko Sao Paulo, mnamo Juni 7 na Juni 18.

Mchezaji huyo pia alihojiwa na polisi kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa mwezi Juni kwa kurusha kwenye mitandao ya kijamii, kudhibitisha kuwa hana hatia, video inayoonyesha mazungumzo kati yake na Najila Trindade.

Neymar, mchezaji ghali zaidi katika historia ya soka duniani, aliwasili kutoka Barcelona kwenda PSG msimu wa joto wa mwaka 2017 kwa rekodi ya jumla ya Euro milioni 222, anapitia mwaka huu na wakati mgumu pia katika suala la michezo.

Neymar ameendelea kuweka wazi nia yake ya kurudi Barcelona.

Neymar ambaye ana jeraha kwenye mguu, hakuweza kuambatana na timu yake kushiriki katika michuano ya Copa America mnamo mwezi Julai, ambapo vijana wa Seleçao walitwaa taji.