BARCELONA-JUVENTUS-PSG-SOKA

Barcelona na Juventus wamtaka Neymar

Neymar, mshambuliaji wa klabu ya PSG.
Neymar, mshambuliaji wa klabu ya PSG. REUTERS/Charles Platiau

Vyombo vya habari vya michezo vimeripoti kuwa Barcelona inatarajiwa kuwasilisha ombi la kuutaka uongozi wa klabu ya ufaransa Paris St-Germain kusaini makubaliano ya kujiunga ingawa kwa mkopo na mshambuliaji wa klabu hiyo Neymar, 27, kutoka wiki hii kukiwa na fursa ya kuyafanya makubaliano hayo kuwa ya kudumu.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imetolewa kukiwa na tetesi kwamba Juventus na yenyewe imeanza mazungumzo na PSG katika harakati za kutaka kumsaini mshambuliaji wa klabu hiyo Neymar, ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Ufaransa kwa dau la pauni milioni mia mbili mwaka 2017.

Barcelona haijajiandaa kuachilia ndoto yake ya kumrudisha Nou Camp mchezaji huyo wa Brazil.

PSG iko tayari kuipatia Real Madrid mshambuliaji wake Neymar iwapo klabu hiyo itawapatia beki wake wa kati Raphael Varane, 26, na winga mwenye umri wa miaka 19 Vinicius Jr.

Wakati huo huo Bayern Munich imemsajili mshambuliaji wa kiungo wa kati Philippe Coutinho kutoka Barcelona kwa mkopo msimu mpya inayojumuisha uwezekano wa kumnunua.

Barcelona inasema timu ya Ujerumani italipa Euro milioni 8.5 kumchukua mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 27, kwa mkopo huku kukiwa na fursa ya kumnunua kwa kititia cha Euro milioni 120.