Pata taarifa kuu
SOKA-LIGI KUU-WACHEZAJI-TUZO

Joash Onyango mchezaji bora nchini Kenya

Beki wa Gor Mahia Joash Onyango
Beki wa Gor Mahia Joash Onyango @OfficialGMFC
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Beki wa klabu ya Gor Mahia nchini Kenya Joash Onyango, ndiye mchezaji bora wa msimu wa 2018/2019 katika lgi kuu ya soka nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Onyango ambaye pia ni beki wa timu ya taifa Harambee Stars, alipata tuzo hiyo kutoka kwa muungano wa wanahabari wa michezo nchini humo (SJAK) ambayo hutoa taji hilo kila mwaka.

Mbali na tuzo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye alishinda pia tuzo ya beki bora, alikabidhiwa pia kitika cha Dola 10,000 sawa na Shilingi za nchi hiyo Milioni 1.

Wachezaji wengine waliokuwa wanapambania tuzo hiyo ni pamoja na mchezaji wa zamani wa Gor Mahia Francis Kahata, ambaye siku hizi, anaichezea Simba SC nchini Tanzania na Enosh Ochieng.

Wachezaji wengine walioshinda mataji:-

Mchezaji bora wa mwaka: Joash Onyango -Gor Mahia

Kipa bora: 1.Faruk Shikalo (Bandari), 2. Justine Ndikumana (Sofapaka), 3.Samuel Odhiambo (Western Stima);

Beki bora: 1.Joash Onyango (Gor Mahia), Kelvin Wesonga (Sony Sugar), Brian Otieno (Bandari FC).

Kiungo wa Kati: 1.Francis Kahata (Gor Mahia), Abdalla Hassan (Bandari FC), Cliff Nyakeya (Mathare United);

Mfungaji bora:1.Enosh Ochieng-Magoli 20 , (Ulinzi Stars), Allan Wanga- Magoli 18, (Kakamega Homeboyz), Umaru Kasumba-Magoli 17 (Sofapaka).

Mchezaji chipukizi:-1.David Majaka (Tusker FC), Jackson Dwang (Nzoia FC), Daniel Sakari (Kakamega Homeboyz),

Kocha bora wa mwaka:- 1.Hassan Oktay (Gor Mahia), Bernard Mwalala (Bandari FC), John Baraza (Sofapaka).

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.