Pata taarifa kuu
KENYA-HISTORIA-MAKOCHA-SOKA

Wafahamu makocha waliowahi kufunza soka nchini Kenya

Aliyewahi kuwa kocha wa Kenya Adel Amrouche, raia wa Algeria na Ubelgiji
Aliyewahi kuwa kocha wa Kenya Adel Amrouche, raia wa Algeria na Ubelgiji FKF

Francis Kimanzi ameingia katika orodha ya makocha zaidi ya 30 watakaokumbukwa kuifunza timu ya taifa Harambee Stars, katika historia yake ya mchezo wa soka.

Matangazo ya kibiashara

Kimanzi, anaingia katika orodha ya makocha wengine wazawa kama vile Mohammed Kheri, Jacob “Ghost” Mulee na Twahir Muhiddin ambao wamekuwa wakifutwa kazi na kurejeshwa tena kuifunza Harambee Stars.

Mkenya wa kwanza kuifunza Harambee Stars, alikuwa ni Elijah Lidonde, aliyepwa mikoba ya timu ya taifa mwaka mwaka 1967.

Baadaye Jonathan Niva alipewa kazi hiyo mwaka 1972, Stephen Yongo (1979) na Marshal Mulwa ( 1980-83).

Makocha wengine wazawa waliowahi kuifunza Harambee Stars ni pamoja na, Christopher Makokha (1988), Mohammed Kheri (1988-90, 1995, 2005), Abdul Majid (1998), James Siang'a (1999-2000).

Joe Kadenge (2002), Jacob Ghost Mulee (2003-04, 2007-08, 2010) , Twahir Muhiddin (2004-2005, 2009-2010), Tom Olaba 2006, Musa Otieno (2010-2011), Francis Kimanzi (2008-09, 2011-12, 2019-) na Stanley Okumbi (2016-17,2018 ).

Hata hivyo, Albert Henry Gibbons raia wa Uingereza, alikuwa kocha wa kwanza wa kigeni, kuifunza Harambee Stars, kati ya mwaka 1966-1967.

Marehemu Reinhard Fabisch kutoka Ujerumani, anaendelea kukumbukwa sana kwa namna alivyobadilisha soka katika timu ya taifa na kuwaleta vijana chipukizi wakati alipokuwa kocha kati ya mwaka 1987, 1997 na baadaye kati ya 2001-2002.

Wengine ni pamoja na Mjerumani Eckhard Krautzun (1971) , Ray Wood kutoka Uingereza (1975), Grzegorz Polakow (Poland) mwaka 1975.

Bernhard Zgoll raia wa Poland-Ujerumani mwaka 1984, Reinhard Fabisch

Gerry Saurer naye alipewa kazi mwaka 1992, Vojo Gardašević kutoka Yugoslavia mwaka 1996, Christian Chukwu-Mnaigeria 1998, Bernard Lama Mfaransa, mwaka 2006.

Antoine Hey Mjerumani, 2009, Henri Michel Mfaransa-2012-2013, Adel Amrouche (Algeria) 2013-2014, Bobby Williamson kutoka Scotalnd, kati ya mwaka 2014-2016, Paul Put Mbelgiji 2017-2018 na raia wa Ufaransa Sébastien Migné 2018-2019.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.