Pata taarifa kuu
KENYA-SOKA-MICHEZO

Sintofahamu yaibuka siku chache kabla ya uchaguzi wa kiongozi wa Shirikisho la soka Kenya

Sebastian Migne (Kushoto) kocha mpya wa Harambee Stars, akitambulishwa rasmi na rais wa Shirikisho la soka nchini Kenya FKF Nick Mwendwa (Katikati) jijini Nairobi Mei 03 2018
Sebastian Migne (Kushoto) kocha mpya wa Harambee Stars, akitambulishwa rasmi na rais wa Shirikisho la soka nchini Kenya FKF Nick Mwendwa (Katikati) jijini Nairobi Mei 03 2018 FKF
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Rais wa Shirikisho la soka nchini Kenya Nick Mwendwa, alikuwa ni mgombea pekee, aliyewasilisha fomu zake kwa bodi inayoandaa uchaguzi wa kiongozi wa soka nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Wagombea wengine, wakiongozwa na rais wa zamani Sam Nyamweya, Moses Akaranga, Alex Ole Magelo na Steve Mburu hawakujitokeza kwa madai kuwa, bodi itakayosimamia uchaguzi huo, ilibadilisha sheria ili kumpendelea Mwendwa.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa bodi Edwin Wamukoya amesisitiza kuwa, siku ya Jumatano ilikuwa ya mwisho kwa walionesha nia kurudisha fomu zao na sasa mlango umefungwa.

Nyamweya amelimbia Gazeti la Daily Nation kuwa, malalamishi yao yako Mahakamani na kamati maalum inayoshughulikia masuala ya michezo nchini humo na anaamini kuwa madai yao yatashughulikiwa.

“Tutawasilisha fomu zetu, baada ya Mahakama kutusikiliza na kuamua suala hili, bado tupo kwenye kinyang'anyiro hicho,” amesema Nyamweya.

Mgombea mwingine, Ale Ole Magelo amesema, wanachotaka ni nafasi sawa, kwa kila mmoja kushiriki katika uchaguzi huo na iwapo itabidi kupata msaada wa Shirikisho la soka duniani FIFA.

Uchaguzi wa kiongozi wa Shirikisho la soka nchini humo, umepangwa kufanyika tarehe 7 mwezi Desemba jijini Nairobi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.