Pata taarifa kuu
SOKA-MISRI-VIJANA

Michuano ya Vijana barani Afrika yaanza nchini Misri

Uwanja wa soka
Uwanja wa soka Signify
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Makala ya tatu ya mchezo wa soka, kutafuta bingwa wa Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 23, inaanza kutifua vumbi nchini Misri, siku ya Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Michuano hii, inatarajiwa kumalizika tarehe 22 mwezi Novemba.

Timu zitakazomaliza katika nafasi tatu bora, zitafuzu katika michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwaka 2020 jijini Tokyo nchini Japan.

Nigeria ndio mabingwa watetezi wa taji hili. Mwaka 2015, michuano hii ilifanyika jijini Dakar nchini Senegal.

Mataifa yanayoshiriki ni pamoja na wenyeji Misri, Cameroon, Ghana, Ivory Coast, Mali, Nigeria, Afrika Kusini na Zambia.

Makundi:

Kundi la A : Misri, Mali, Cameroon na Ghana

Kundi B: Nigeria, Ivory Coast, Afrika Kusini na Zambia.

Ratiba ya Ijumaa

Misri vs Mali

Cameroon vs Ghana

Ratiba ya Jumamosi

Nigeria vs Ivory Coast

Afrika Kusini vs Zambia

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.