UINGEREZA-TOTTENHAM-SOKA

José Mourinho ateuliwa kuwa kocha wa klabu ya Uingereza ya Tottenham

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho wakati wa mechi dhidi ya Tottenham kwenye uwanja wa Old Trafford, Manchester Agosti 27, 2018.
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho wakati wa mechi dhidi ya Tottenham kwenye uwanja wa Old Trafford, Manchester Agosti 27, 2018. REUTERS/Andrew Yates

Kocha maarufu kutoka Ureno, José Mourinho, atachukua nafasi ya Mauricio Pochettino kutoka Argentina, ambaye aliongoza Spurs katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka jana.

Matangazo ya kibiashara

Mourinho amekuwa nje ya ukufunzi kwa takriban mwaka mmoja sasa, na huku akiendelea kuishi mjini London.

Pochettino mwenye umri wa miaka 47 alifutwa kazi kama mkufunzi wa Spurs Jumanne usiku baada ya kuhudumu katika klabu hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.

Msimu huu umeanza vibaya, ambapo Tottenham imekuwa ikipata vipigo vya mara kwa mara, ikiwemo kipigo cha 7-2 kutoka kwa Bayern Munich mwezi uliopita.

Kumekuwa na ripoti kuhusu mvutano kati ya Pochettino na mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy. Hali ambayo imewalazimu wakuu wa Spurs kumfuta kazi Pochettino na kutafuta usaidizi wa José Mourinho.