AFCON 2021-CAMEROON-CAF-SOKA

Cameroon yakubali kuwa mwenyeji wa AFCON 2021

Rais wa Shirikisho la Soka (CAF) Ahmad na mshauri wake na nyota wa zamani Samuel Eto'o.
Rais wa Shirikisho la Soka (CAF) Ahmad na mshauri wake na nyota wa zamani Samuel Eto'o. ISSOUF SANOGO / AFP

Awamu inayofuata ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) hatimaye itachezwa nchini Cameroon kuanzia Januari 9 hadi Februari 6 badala ya Juni / Julai.

Matangazo ya kibiashara

Jumatatu hii Januari 15, mamlaka nchini Cameroon na Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) wamekubaliana kuhusu mabadiliko ya tarehe hizo jijini Yaounde, kutokana na msimu wa mvua katika ukanda huo.

Mabadiliko haya bado yanatarajiwa kujadiliwa tena katika mkutano utakaofuata wa Kamati tendaji ya CAF, ambao utafanyika kando ya michuano ya Kombe la Afrika la Futsal (kuanzia Januari 28 hadi Februari 7 huko Laayoune).

Hoja hii imepitishwa kutokana na suala la hali ya hewa "katika majira ya joto" nchini cameroon.

Uamuzi huu pia unaweza kupitishwa upya kwa michuano ya AFCON 2023 nchini Cote d'Ivoire na michuano ya AFCON 2025 nchini Guinea, kwa vile pia itakuwa msimu wa mvua katika eneo la Afrika Magharibi.