Lyon yamsajili mshambiliaji kutoka Zimbabwe Tino Kadewere
Imechapishwa:
Klabu ya Ufaransa Le Havre imetangaza kwamba imemaliza makubaliano ya kumuuza mchezaji wake Tino Kadewere kutoka Zimbabwe kwa timu ya Lyon inayoshirikimichuano ya daraja la kwanza.
Hata hivyo, Kadewere, mfungaji bora wa msimu huu katika michuano ya daraja la pili, ambaye amekwisha funga mabao 18, ataendelea kuichezea klabu yake Le Havre hadi mwisho wa msimu.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 anasemekana amesaini mkataba wa miaka minne na nusu kwa dola za Marekani milioni 16.6.
Kadawere, ambaye pia alichezea klabu ya Djugardens, nchini Sweden, ameshiriki michuano 15 ya kimataifa.
Alikuwa pia sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya soka ya Zimbabwe, Warriors, kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka jana nchini Misri.