CAF-SOKA-MICHEZO

Timu mbalimbali kujitupa viwanjani mwishoni mwa wiki hii

Wachezaji wa TP Mazembe wakisherehekea ushindi wao wa Kombe la Shirikisho Jumapili Novemba 6 huko Lubumbashi.
Wachezaji wa TP Mazembe wakisherehekea ushindi wao wa Kombe la Shirikisho Jumapili Novemba 6 huko Lubumbashi. STRINGER / AFP

Mzunguko wa tano, kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika unachezwa mwishoni mwa wiki hii katika viwanja mbalimbali barani Afrika. Siku ya Ijumaa, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inayoongoza kundi la A kwa alama 10, ipo ugenini kucheza na Zamalek ya Misri.

Matangazo ya kibiashara

Mechi hii inachezwa katika uwanja wa Al Salam jijini Cairo na matokeo katika mechi hii, yatatoa mustakali wa kundi hili ambalo Zamalek ina alama 7.

Mabingwa hao wa zamani, wameshinda mechi tatu kati ya nne walizocheza.

Siku ya Jumamosi,ZESCO United ya Zambia na Clube Desportivo de Agosto ya Angola ambazo zina alama, zitamenyana katika uwanja wa Levy Mwanawasa jijini Ndola.

Kundi B, Etoile du Sahel ya Tunisia ambayo ina alama tisa, itakuwa katika uwanja wa Al Salam jijini Cairo, kumenyana na wenyeji wao Al-Ahly ambayo wana alama saba.

FC Platinum ya Zimbabwe ambayo haina matumaini ya kusonga mbele katka michuano hii, itakuwa inajaribu kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Al-Hilal ya Sudan ambayo ina alama sita, katika uwanja wa Barbourfields mjini Bulawayo siku ya Jumamosi.

Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambayo inaongoza kundi la C kwa alama 10, siku ya Jumamosi itakuwa mgeni wa Petro de Luanda ya Angola, huku Wydad Casablanca ya Morocco ikiikaribisha USM Alger, katika uwanja wa Mohammed V mjini Casablanca.

Esperance de Tunis ya Tunisia na Raja Casablanca siku ya Jumamosi, zitakuwa zinatafuta kiongozi wa kundi D, katika mechi inayotarajiwa kuwa ngumu itakayochezwa mjini Rades.

AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itakuwa mwenyeji wa JS Kabylie ya Algeria jijini Kinshasa. JS Kabylie ina alama nne huku AS Vita Club ikiwa na alama moja baada ya kupoteza mechi tatu na kwenda sare mara moja.