MAREKANI-MPIRA WA KIKAPU-MICHEZO

Nyota wa mpira wa kikapu Kobe Bryant afariki katika ajali ya helikopta

Katika misimu 20 ya NBA, Kobe Bryant alifunga mali zaidi na kuandikisha alama 33,643.
Katika misimu 20 ya NBA, Kobe Bryant alifunga mali zaidi na kuandikisha alama 33,643. REUTERS/Lucy Nicholson

Mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu Kobe Bryant, ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji bora kwa misimu yote, amefariki dunia katika ajali ya helikopta, tovuti ya Marekani ya TMZ imeripoti. Kobe Bryant alikuwa na umri wa miaka 41.

Matangazo ya kibiashara

Mchezaji wa zamani wa Lakers na Mchezaji nguli wa mpira wa kikapu Kobe Bryant alifariki Jumapili asubuhi Januari 26 katika ajali ya helikopta yake ya binafsi huko Calabasas, kusini mwa California, kulingana na tovuti ya habari ya Marekani ya TMZ. Taarifa hii imethibitishwa baadae na mamlaka ya eneo hilo.

Hata hivyo kuna taarifa ambazo zimebaini kwamba nyota wa mpira wa kipaku nchini Marekani Kobe Bryant na binti yake Gianna ni miongoni mwa watu tisa waliofariki katika ajali ya helkopta iliyotokea mji wa Calabasas, California.

Ripoti za awali zilisema kuwa kulikuwa na watu watano ndani ya ndege.

Kobe Bryant, mwenye umri wa miaka 41, alichezea NBA ya Los Angeles Lakers kwa miaka 20. Kobe Bryant ambaye alikuwa bingwa wa NBA mara tano, ni mmoja wa wachezaji saba aliyefunga zaidi na kuandikisha alama 30,000 na kuchukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji bora kwa kipindi chote alipokuwa akicheza.

Sababu za ajali ya helikopta hiyo bado hazijajulikana. Mamlaka inasema jumla ya watu wanane waliokuwa katika helikopta hiyo, ikiwa ni pamoja na rubani, hakuna aliyenusurika ajali hiyo.

Bryant alikuwa hadi Jumamosi Januari 25 mfungaji wa tatu bora katika historia ya NBA, kabla ya kuangushwa na mpinzani wake LeBron James wakati wa Lakers iliposhindwa huko Philadelphia (108-91).