GUINEA-AJALI-SOKA

Serikali ya Guinea yawalilia wachezaji wa mpira waliofariki katika ajali ya barabarani

Guinea itaendelea kuwakulbuka wachezaji wa klabu ya Étoile de Guinée kufariki dunia katika ajali ya barabarani Machi 5, 2020.
Guinea itaendelea kuwakulbuka wachezaji wa klabu ya Étoile de Guinée kufariki dunia katika ajali ya barabarani Machi 5, 2020. Tim Clayton/Corbis via Getty Images

Serikali imetangaza maombolezo ya kitaifa baada ya wachezaji wa mpira wa miguu kufariki dunia katika ajali ya barabarani.Timu ya soka ya Étoile de Guinée, ilikuwa njiani kushirikia mchezo wa daraja la pili wakati ajali ilitokea Alhamisi Machi 5.

Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kitaifa la kuaga miili ya wachezaji kumi waliofariki katika ajali hiyo lilifanyika Jumatatu hii asubuhi katika uwanja wa Septemba 28.

Mazishi ya wachezaji hao yamefanyika leo Jumatatu, baada ya sala ya maiti katika msikiti mkubwa wa Fayçal.

Wakati wa zoezi la kuaga miili ya wachezaji hao kumi watu waliokuja kutoa heshima zao za mwisho walionekana wakiwa na huzuni, huku wengine wakigalagala chini kwa vilio, muda mfupi baada ya kutajwa majina ya wahanga na kuonyesha jeneza ambamo walihifadhiwa zilizofunikwa na bendera ya taifa la Guinea.

Wachezaji wanane walifariki dunia, pamoja na dereva na daktari wa timu hiyo ya Étoile de Guinée.