SENEGAL-MICHEZO

Michezo ya Olimpiki kwa vijana mwaka 2022 Dakar yaahirishwa

Kuahirishwa kwa michezo hiyo ni pigo kubwa kwa vijana. La Dakar Arena de Diamniadio.
Kuahirishwa kwa michezo hiyo ni pigo kubwa kwa vijana. La Dakar Arena de Diamniadio. RFI / Pierre René-Worms

Michezo ya olimpki kwa wanariadha walio na umri kati ya 15 na 18, imeahirishwa hadi mwaka 2026 barani Afrika. ingelikuwa Michezo ya kwanza ya Olimpiki iliyoandaliwa katika bara hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kuahirishwa kwa michezo hiyo kulitokana na janga la Covid-19 linaloendelea kushika kasi katika mataifa mbalimbali duniani. Janaga hili limesabaratisha kalenda ya michezo ya kimataifa.

Baada ya Tokyo mnamo mwaka 2021, mwaka 2024 kuna mashindano ya Olimpiki ya Majira ya Paris yatakayofanyika. mwaka 2028 pia, kuna Michezo ya Los Angeles. unasalia mwaka 2026 tu, "ambapo kuna viwanja ambavyo vinaweza kupatikana", amebaini rais wa Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki nchini Senegal Mamadou Diagna Ndiaye.

Uamuzi "ambao unakidhi matakwa ya uwajibikaji na haja ya ufanisi," kulingana na maafisa wa kamati ya maandalizi ya michezo hiyo kutoka Senegal, ambao walifanya mkutano na waandishi wa habari Alhamisi wiki hii.

Kuahirishwa kwa michezo hiyo ni pigo kubwa kwa vijana.

"Uamuzi ambao ulichukuliwa kwa pamoja na Senegal na Kamati ya kimataifa ya Michezo ya Olimpki, IOC, haukutokana na kucheleweshwa kwa maandalizi ya Michezo. Ni jambo la kawaida katika ajenda ya michezo ya Olimpiki. Tulikuwa tayari kutekeleza yote kwa wakati, " amesema rais wa Kamati ya kitaifa ya Olimpiki nchini Senegal Mamadou Diagna Ndiaye.

Vijana 4000 walio na umri wa miaka kati ya 15 na 18 kutoka nchi zaidi ya 200 walitarajiwa kushiriki mashindano haya nchiniSenegal. Kufikia 2026, wanariadha hawa watakuwa wamezidi umri wa miaka ya kushiriki mashindano hayo. Ibrahima Wade, mratibu wa Michezo ya Olimpiki ya Vijana, anasema anaelewa kilio cha vijana hao, lakini "bado tunayo nafasi kwa vijana hawa: Michezo ya Vijana barani Afrika, ambayo itaandaliwa Lesotho mnamo mwaka 2022. Sio Michezo ya Olimpiki. , lakini ni fursa ya kutetea bendera ya taifa la Senegal kwa barani Afrika."

Kamati ya kitaifa ya Olimpiki pia imesema inafikiria kuandaa michezo mingine, "kuwapima nguvu wanariadha vijana".