COTE D'IVOIRE-SOKA

Côte d’Ivoire: Mchakato wa uchaguzi wa kiongozi wa FIF wasitishwa, Drogba kusubiri

Didier Drogba (katikati), wakati akiwasilisha maombi yake ya kuwani kwenye kiti cha uongozi wa Shirikisho la Soka la Côte d’Ivoire.
Didier Drogba (katikati), wakati akiwasilisha maombi yake ya kuwani kwenye kiti cha uongozi wa Shirikisho la Soka la Côte d’Ivoire. SIA KAMBOU / AFP

Shirikisho la Mpira wa Miguu la Côte d’Ivoire (FIF) limeamua kusitisha mchakato wa kumteua kiongozi wake mpya hadi pale mkutano mkuu wa shirikisho hilo utafanyika.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo ulitarajiwa kufanyika Agosti 29, 2020. FIF inabaini kwamba Tume ya Uchaguzi inayohusika na kujadili faili za mgombea haikuwajibika kwa kazi zake. Tangu saa 72 zilizopita, wasaidizi wa nyota wa zamani wa soka Didier Drogba wanahakikisha kwamba mchezaji huyo wa zamani amekubaliwa kuwania kwenye nafasi hiyo.

Agosti 12, 2020, mzozo katika Shirikisho la Soka la Côte d’Ivoire (FIF), ambao umedumu kwa miaka mitatu, umeingiliwa na jaribio lingine. Uchaguzi wa rais wake mpya, ambaye ulikuwa umepangwa, hautafanyika Septemba 5, 2020. Kamati ya Dharura ya IFF imeamuru "kusitisha mchakato wa uchaguzi" na "kuitisha mkutano mkuu […] Jumamosi Agosti 29, 2020 jijini Abidjan ”, iimebaini taarifa iliyoandikwa Agosti 11.

'Mapungufu mkubwa katika mchakato wa uchaguzi'

Kamati ya Dharura, ambayo inaundwa na vigogo zaidi wa Shirikisho la soka la Côte d’Ivoire (ikiwa ni pamoja na kiongozi anyemaliza muda wake Sidy Diallo), imebaini kwamba "Tume ya uchaguzi", ilyowekwa na kuongozwa na waziri wa zamani wa michezo René Diby, "ilikiuka sheria za uchaguzi za FIF na mamlaka aliyopewa na Mkutano Mkuu".

René Diby analaumiwa kwa jinsi alishindwa kuwajibika katika kupitisha majina wa watu wanne kuwania kwenye nafasi hiyo.

Vyombo kadhaa vya habari vinabaini kwamba René Diby alipata shinikizo ili aweze kupitisha majina ya watu hao wanne agosti 9, 2020.